Habari Mpya

Powered by Blogger.

Videos

KITAIFA

KIMATAIFA

BIASHARA

KILIMO

HABARI PICHA

» » WAKURD WAILALAMIKIA TURUKI
Unknown

KIKOSI cha wapiganaji wa Kikurdi kaskazini mwa Syria kimeishtumu Uturuki kwa kuwashambulia wanajeshi wake mara kwa mara karibu na mpaka.
Kinasema kuwa vifaru vya Uturuki vimeshambulia eneo moja linalodhibitiwa na vikosi hivyo karibu na mji wa Jarablus huku gari lake moja likilipuliwa karibu na Kobane.
Uturuki imesema kuwa inachanguza madai hayo.
Imesisitiza kuwa oparesheni yake inayoendelea haijawalenga Wakurdi wa Syria pamoja na kundi la kikurdi la PKK nchini Iraq.
Wakati huohuo Waziri Mkuu nchini Uturuki, Ahmet Davotuglu amepinga kupelekwa kwa wanajeshi wa ardhini ili kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State.
Maofisa wa polisi nchini Uturuki wameendelea kuwakamata wanachama wa kundi la IS na wale wa PKK wanaoshukiwa katika uvamizi.
#BBC

«
Mbele
DR SLAA AKANUSHA UZUSHI WA WANAODAI KUKIHAMA CHADEMA
»
Nyuma
LOWASA ATIKISA CCM WAJIHAMI KUZUIA KUNDI LINALOHAMA KWA NGUVU