Rushwa hii ya Magufuli haitafautiani na ile ya Maisha Bora kwa kasi mpya.
Baada ya magufuli kusema pale dodoma kuwa hata waangusha wana ccm,kisha akasema anajua shida za watanzania,kisha akaja na Kutetea waendesha bodaboda na mama ntilie,alipofeli sasa amekuja na rushwa ya kugawa laptop kwa waalimu kwa maneno na kusambaza milioni 50 kila kijiji,hii inaonyesha udhaifu mkubwa wa magufuli na wapambe wake,ndiyo maana wamebakia na masengenyo ya kufitini mgombea wa Ukawa kwa kujionyesa kuwa wao ni wasafi wasiyo na hatia,wanasahau kuwa hao anaowadanganya ndiyo wanaomkataa,na hao wanao mchagua wanayemtaka ndio anaotaka kuwapa ahadi ya Rushwa ya maneno ambayo hayana mashiko,sisi wana wa kitanganyika na Zanzibar tunataka mabadiliko. Na Waalimu hawataki Laptops wanataka kuboreshewa maisha wathaminiwe kama wanasiasa walivyojikinai wanavyo jithamini hadi kufikia hatua ya kukatalia Ikulu,sasa ni wakati wa kuondoa ujinga na kuanza upya siyo wakati wa kudanganyana.Maisha ya bahadi ziliishia 2010 sasa ni mwendo wa kushoma na kufuta ccm ndiyo kauli ya waalimu.
Imeelekezwa: Kitaifa