Habari Mpya

Powered by Blogger.

Videos

KITAIFA

KIMATAIFA

BIASHARA

KILIMO

HABARI PICHA

» » STAMICO YAONGEZA UKUSANYAJI MAPATO

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeongeza ukusanyaji wa mapato yatokanayo na uwekezaji hadi kufikia Sh bilioni 3.17 kwa mwaka mmoja tangu kuboreshwa upya kwa shirika hilo.
Akizungumzia mafanikio ya shirika hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Zena Kongoi alisema kiasi hicho kimepatikana kutokana na uwekezaji kupitia kampuni zake tanzu na utoaji wa huduma za kibiashara kutoka Sh milioni 281 kwa mwaka 2013/14.
Lengo la Shirika lilikuwa ni kukusanya Sh bilioni 5 hadi ifikapo Juni wa mwaka wa fedha 2014/15. “Lengo tulilowekewa na Wizara ya Nishati na Madini ni kuhakikisha tunakusanya jumla ya Sh bilioni 200 kwa mwaka ifikapo mwaka 2016.
Lakini mikakati ya Shirika kwa miaka mitano ya kuanzia mwaka 2014/15 hadi mwaka 2018/19 ni kuweza kukusanya Sh bilioni 50 kwa mwaka,” alisema. Kongoi alisema shirika hilo pia limefanikiwa kusainiwa kwa Hati ya Marekebisho ya Uanzishwaji wa shirika, kufufua na kuimarisha huduma za uchorongaji wa miamba, utafiti wa madini na utoaji ushauri wa kijiolojia na uchimbaji madini kwa migodi mikubwa, ya kati na ya wachimbaji wadogo.
“ Shirika limefanikiwa kuchoronga mita 2434 za aina ya diamond na mita 8,000 za aina ya Reverse Circulation ambazo zimeingizia shirika Sh bilioni 1.81 na sasa tuko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha kupata mkopo wa dola za Marekani 790,000 kutoka benki ya TIB kwa ajili ya kununulia mitambo miwili mipya ya kuchorongea ambayo itawasaidia wachimbaji wadogo wa hapa nchini,” alisema.
Kuhusiana na uzalishaji wa dhahabu kupitia kampuni tanzu ya STAMIGOLD Biharamulo, Kongoi alisema wameweza kuzindua mkuo wa kwanza wa dhahabu wa kilo 25 wenye thamani ya Sh bilioni 1.5 na kusafirisha na kuuza nchini Uswisi kiasi cha wakia 12,923.35 za dhahabu na kuingizia kampuni na taifa dola za Marekani milioni 15.6.
Akizungumzia mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira uliorejeshwa kwa shirika hilo, Kongoi alisema shirika liko katika hatua za mwisho za zabuni ya kumpata mwekezaji mbia kwa ajili ya kuendesha mgodi huo na kuongeza kuwa shirika limepeleka timu ya uangalizi na wasimamizi katika mgodi wa tanzanite wa Mirerani, ikiwa ni katika kusimamia maslahi ya taifa katika miradi ambayo serikali imeingia ubia na wawekezaji.#Habarileo

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post