Mhe.Juma Duni Haji,Asema umasikini wa watanzania unafanywa kimakusudi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) ngazi ya Taifa na Waziri wa Afya wa Serikali ya Zanzibar, Mhe.Juma Duni Haji amepitishwa rasmi kuwa Mgombea Mwenza wa Mhe.Edward Lowassa kupitia CHADEMA. Hii ina maana Duni amejiuzulu dhadhifa zote ndani ya serikali na ndani ya chama chake CUF ikiwa ni pamoja na kujivua uanachama wa CUF na kupewa kadi ya uanachama ya CHADEMA. Amesema umasikini wa watanzania ni umasikini wa kimakusudi ili ccm iwatawale watanzania kwa urahisi,amesema hakuna unafuu wa maisha hata kwa waalimu ambao ni kiungo mhimu cha watanzania na dunia nzima,amegusia madai ya adactari wanao daihaki yao na kupigwa mabomu,ameomba wana usalam wajali wana nchi huku wakijua kuwa wananchi ndiyo wanao wafanya kula lakini wanawaua kwa mabomu,ameongeza kusema kuwa umoja wa ukawa ni sehemu ya mabadiliko na wakati ni sasa kuanzia ndani ya familia zetu na hatimaye kuleta mabadiliko.
Imeelekezwa: habari mpya Kitaifa